PAROKIA YA BIKIRA MARIA WA
MLIMA KARMEL - BUNJU
KWAYA YA
BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMEL
JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM
P. O. Box 167, Dar es Salaam
MOBILE: +255784 799 455
RISALA YA KWAYA KATIKA MAADHIMISHO YA SOMO WA KWAYA TAREHE
26.07.2015
|
Utangulizi:
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Baba
Paroko, Mapadre, Ndugu viongozi wa Parokia, Kigango, na viongozi wa vyama vya
kitume. Ndugu Wapendwa Walezi, Marafiki wa Kwaya, Ndugu wa Karibu wa wanakwaya
na wanakwaya wote.
TUMSIFU
YESU KRISTO…………………….
Ni jambo Jema na la kumshukuru
Mungu aliye asili ya mema yote ambaye ametuwezesha kukaa hapa leo na kuweza
kutujaalia nguvu na ushirikiano wa
pamoja wa hali na mali katika Kwaya yetu.
Leo ni siku ambayo tunaadhimisha
Somo na Msimamizi wa Kwaya yetu Bikira Maria wa Mlima Karmeli ambapo huwa
inaadhimishwa Tarehe 16.07 kwa kila mwaka, hivyo kwa furaha kubwa tunapenda
kuwakaribisha ninyi nyote kushiriki nasi katika furaha hiyo kubwa . Tunasema KARIBUNI SANA .
Risala hii imegawanyika katika sehemu zifuatazo:-
1.
HISTORIA FUPI YA KWAYA
Kwaya ya Bikira Maria wa Mlima
Karmeli ilianzishwa mnamo mwaka 1998 ikiwa chini ya Somo na Msimamizi wa Kwaya
Mt. Fransisko wa Asizi ikiwa na wanakwaya waanzilishi 15. Na baadaye
kubadilisha jina na kuwa chini ya Somo na Msimamizi Mama Bikira Maria wa Mlima
Karmeli mnamo mwaka 2012. Kwa sasa Kwaya ina wanakwaya 55 na inaongozwa na
kamati tendaji inayoundwa na viongozi wafuatao:-
- Luambano Patrick – Mwenyekiti
- Isack Ntalyoka – M/ Mwenyekiti
- Sibilina Kimaro – Katibu
- Isack Ntalyoka – M/ Katibu
- Clara Samwel – Mhazini.
Kwaya pia ina Walezi walei
wanane(8) Marafiki wa Kwaya Familia 30.
2. MPANGO KAZI
WA MWAKA 2015/2016
Kwa Mwaka 2015, Kamati
tendaji ya Kwaya na wanakwaya wote wameridhia kuwa na MPANGO KAZI
unaotekelezeka wa mwaka mzima na
kujitahidi kuondoa mgangano/muingiliano wa matukio na vyama vingine vya kitume
ili kuweza kuleta ufanisi zaidi kwa kugawanya
matukio katika sehemu kuu nne kama ifuatavyo:-
Imani na Liturujia
Uimbaji
Uchumi
Mahusiano
1.
IMANI NA LITURUJIA.
v
Katika
kuhakikisha wanakwaya wanapata tafakari juu ya imani na wanahudumu kulingana na
liturujia kamati tendaji inapendekeza kuwa na Mafungo pamoja na semina kwa wanakwaya wote
yatakayo fanyika mara tatu(3) kwa mwaka yaani:-
i.
Kipindi
cha Kwaresma
ii.
Kipindi
cha Maandalizi kukaribia kuadhimisha Somo wa Kwaya Bikira Maria wa Mlima
Karmeli Tarehe 16.07.2015
iii.
Katika
Kipindi cha Majilio.
v
Kwa
Imani yetu Kamati Tendaji tunaamini kuwa ni kwa uweza wa Mungu tu ndio tunaweza
kuhudumu vizuri kadiri ya Liturujia katika Ibada ya Misa Takatifu na Matukio
mbalimbali, Hivyo Kwaya imependekeza
kuwa SALA MAALUMU ili kwa pamoja kuweza kujinyenyekeza katika Uweza wa Mungu
kila kabla ya kutoa Huduma popote pale.
v
Kuhamasisha
na kupanga mikakati ya kuhakikisha kuwa Wankwaya wote wanashiriki Ibada ya Misa
Takatifu na Baba Kardinali siku JUMATATU YA PASAKA ambayo ni siku ya
Wanashikwaka –Jimbo kukutana na Baba Kardinali, Pia kujifunzaa mambo mbalimbali
yahusuyo utume wa Kwaya. 06.04.2015 katika Parokia ya Kipawa.
2. UIMBAJI/MUZIKI.
Kamati tendaji ya Kwaya katika
kuhakikisha tunaboresha uimbaji inapendekeza kufanya mambo yafuatayo:-
A.
Kwa
ushirikiano wa Wanakwaya wote na hasa Kamati ya Ufundi kukusanya na kuandaa VITABU
NA BAHASHA za nakala za nyimbo mbalimbali kulingana na vipindi mbalimbali vya
Liturujia kwa Mwaka mzima. Yaani kuweka
nyimbo katika makundi yafuatayo:-
i.
Nyimbo
za Mwanzo
ii.
Nyimbo
za Misa
iii.
Nyimbo
za Zaburi(Katikati)
iv.
Shangilio
na Maombi
v.
Komunio
na Ekaristi Takatifu
vi.
Sadaka/Matoleo
na Vipaji
vii.
Nyimbo
za Kristu Mfalme, Majilio na Krismasi
viii.
Nyimbo
za Kwaresma Matawi na Pasaka
ix.
Skukrani
na Bikira Maria
x.
Pentekoste
na Kipaimara
xi.
Ubatizo
na Ndoa
xii.
Nyimbo
za Watakatifu, Tafakari na Misa.
B.
Kuandaa
Semina na Mafunzo yanayohusu Elimu ya Muziki, Uongozi na Upimishaji kwa Kamati
ya Ufundi na Wanakwaya wengine watakaohitaij ili kuweza kuboresha zaidi Mazoezi
yetu, Uimbaji wetu na utoaji wa huduma kwa ujumla.
C.
Kuendelea
na zoezi la Kuhamasisha waamini mbalimbali katika Parokia yetu kujiunga na
Kwaya ili kuweza kufikia Idadi ya Wanakwaya 70, Kamati pia inapendekeza zoezi
la Pili la Kuanzia Saa Moja Kamili(1:00) lifufuliwe ili kutoa fursa na Wigo
Mpana wa Kila mwanakwaya kushiriki mazoezi Kikamilifu na kuongeza uwezekano wa
kupata Idadi kubwa ya Wanakwaya wapya.
D.
Kuwa
na Ziara za Uinjilishaji za Mara kwa Mara ili kuimarisha Kwaya Kiumbaji na
kupata fursa ya kujifunza mengi kutoka kwa wenzetu ndani na nje ya Parokia yetu
na hata nje ya Jimbo Letu.
E.
Kuandaa
na Kuanzisha Darasa La Muziki kwa wanakwaya ili kupata Elimu ya kutuwezesha
Kusoma Musiki katika Nota na Kupiga Kinanda.
3. UCHUMI.
Ili kuweza kutengeneza, Kuinua na
Kuimarisha hali ya kiuchumi ya Kwaya na Wanakwaya kwa Ujumla Kamati
inapendekeza yafuatayo yafanyike:-
A.
KUWEKEZA
FEDHA SACCOS
Ndugu wanakwaya, kamati
inapendekeza kuchukua sehemu ya kiasi cha Fedha ya Kwaya iliyopo Benki na
Kuiwekeza Katika Mojawapo ya Saccos zilizopo katika Mazingira yetu ili kuweza
kuiongezea Uwezo wa Kuichumi wa Kwaya, maana Kwa kuweka fedha Saccos inakupa
fursa za Kukopa Mara Tatu(3) ya Amana yako.
B.
KUJIUNGA
KATIKA VIKOBA.
Kamati inapendekeza pia sehemu ya
Mapato ya Fedha inayoendelea kuyapokea tuwekeze katika Mojawapo ya Vikundi vya
Vikoba Vya WAWATA hapa Kanisani. Ili litatupa fursa ya Kupata Faida mwisho wa
Mwaka lakini pia Fursa ya Kukopa kadiri ya Mahitaji yetu kwa kiwango cha Hisa
za Kikundi. Lakini katika hili kamati ilishauri Wanakwaya mmoja mmoja au katika
vikundi nao kujiunga katika Vikoba kwa Imani kuwa ni fursa ya kipekee na yaweza
kuchangia kujikwamua kuichumi na kuboresha mahusiano.
C.
ZIARA
ZA KUUZA ALBAMU ZETU.
Rejea Maelezo ya Sehemu ya 3.D
hapo juu, Kamati inapendekeza pia tuwe na Ziara kwa Lengo la kuendelea Kuuza
Albamu Zetu katika mtiririko ulioelezwa hapo juu.
D.
KUTENGENEZA/KUNUNUA
VITU NA KUVIUZA.
Kwaya imeazimia kuwa Wabunifu kwa
Kutengeneza/ kununua vitu vyenye kuhitajika kwa wanakwaya , familia ya kwaya ya
BMMK na Waamini wenye mapenzi mema ili kuinua na kiimarisha Uchumi. Vifuatavyo
ni Baadhi ya vitu vilivyopendekezwa:-
Kutengeneza
/Kununua Sare ambazo baadhi ya wanakwaya
hawana na kwa ziada ili kununuliwa na wanakwaya Wapya.
Kubuni
Vazi la Familia ya Kwaya ambalo litavaliwa kwenye matukio makubwa ya kwaya yetu
Mf. Sherehe ya Maadhimisho ya Somo wa Kwaya n.k. Na litavaliwa na Wanakwaya
Wote, Walezi wa Kwaya, Marafiki wa Kwaya na Familia ya Mwanakwaya yaani
Mke/Mme/Mtoto/Mlezi…
E.
KUANDAA
ALBAMU YA AUDIO NA VIDEO
Katika mwaka kipindi hichi cha mwaka
Kwaya imepanga kupanua wigo wa Uinjilishaji kwa Kuandaa Albamu ya Audio na
Video. Ambapo Jedwari hapo chini laonesha mchanganuo wa gharama zake:-
A:
KUREKODI ALBAMU YA AUDIO
|
B:
KUREKODI ALBAMU YA VIDEO
|
|||||
S/No.
|
MAHITAJI
|
GRARAMA(Tshs.)
|
S/No.
|
MAHITAJI
|
GRARAMA(Tshs.)
|
|
1
|
NYIMBO 10@20,000
|
200,000
|
1
|
MWALIMU WA STAILI/STEP
|
500,000
|
|
2
|
STUDIO
|
600,000
|
2
|
STUDIO
|
3,000,000
|
|
3
|
KUKODI KINANDA
|
150,000
|
3
|
MAVAZI(SARE) JOZI 4 X 55@40,000
|
8,800,000
|
|
4
|
MPIGA KINANDA
|
150,000
|
4
|
SEHEMU ZA KUREKODIA
|
500,000
|
|
5
|
NAULI KWENDA STUDIO
|
100,000
|
5
|
USAFIRI KWA SIKU 3@200,000/=
|
600,000
|
|
6
|
CHAKULA STUDIO 55@2000
|
110,000
|
6
|
CHAKULA KWA SIKU 4 *55@4000
|
880,000
|
|
7
|
DHARULA
|
90,000
|
7
|
JENERETA NA MUSIKI
|
300,000
|
|
8
|
DHARULA
|
420,000
|
||||
JUMLA
|
1,400,000
|
JUMLA
|
15,000,000
|
4. MAHUSIANO.
Kamati inapendekeza yafuatayo
yafanyike ili kuamsha na kuboresha mahusiano kati ya :-
§
Wanakwaya
Wenyewe
§
Wanakwaya,
Walezi, Marafiki na Familia za Kwaya.
§
Wanakwaya
na Waamini wote/ Jamii yote ndani na nje ya Parokia yetu.
A. KUAMSHA
NA KUBORESHA KIKUNDI CHA MARAFIKI WA KWAYA.
Kamati inapendekeza kuamsha kundi
la Marafiki wa Kwaya kwa wale waliolala na pia kuboresha kwa kuongeza Idadi yao
na kuwashirikisha Matukio na Mambo mbalimbali ya Kwaya kwa njia ya UTANDAWAZI.
Hivyo kwaya imeridhia kufanya yafuatayo:-
·
Kuwa
na Nembo ya Kwaya yenye kujumuisha Anuani ya Kwaya, Barua pepe na Namba za simu
·
Kuwa
na E- mail ya Kwaya.
·
Kuwa
na Blog ya Kwaya ambayo itakuwa na vitu vifuatavyo:-
i.
Picha
na video za Matukio Mbalimbali ya Kwaya
ii.
Picha
za Wanakwaya, Walezi, Marafiki na Majina yao
iii.
Kauli
mbiu ya Kila Mwanakwaya
iv.
Katiba
ya Kwaya
v.
Historia
ya Kwaya
vi.
Albamu
za Kwaya na Miradi yake
vii.
Ratiba
za Matukio mbalimbali ya Kwaya Mf. Ibada n.k
viii.
Na
vinginevyo vingi.
3. MAFANIKIO
YA KWAYA KWA KIPINDI CHA 2015/2016.
A.
UBORESHAJI WA UIMBAJI.
Katika jambo hilo Kwaya
imefanikiwa kuanzisha Darasa la Muziki na baada ya kusuasua na Mkufunzi wa
kwanza kamati tendaji kupitia kwa Mwenyekiti ilifanya maamuzi ya kubadilisha
mwalimu ambapo kwa sasa Mwl. Anthony Kasomangila ndiye anaendelea kufanya mafunzo
katika Darasa hilo.
Katika kufanikisha mpango kazi huo Kwaya
inamwezesha Mwalimu wa Darasa hilo la Muziki jumla kiasi cha Tshs. 100,000/=
kwa mwezi, kwa kipindi cha miezi miwili katika mchanganuo ufuatao:-
1. Kwa
kuwa tayari wanafunzi 16 tayari wameshajiandikisha na kuanza kusoma, hivyo kila
mmoja anapaswa kuchanga Tshs. 5000/= ili kupata 16@5,000/ = 80,000/=.
2. Na
katika Mfuko wa Kwaya tutatoa Tshs. 20,000/= kwa mwezi kwa kipindi cha miezi
miwili. Ambao ndio muda wa kozi hiyo.
B.
MAFUNGO YA KWAYA.
Tulifanikiwa kufanya mafungo ya
Kwaya ambapo yaliongozwa na Padre mnamo Tarehe 16.05.2015 na yalifanyika
nyumbani kwa Rafiki wa Kwaya Mama Theresia Amon.
- KUSHIRIKI ADHIMISHO LA MISA YA WANAKWAYA JIMBO JUMATATU YA PASAKA.
Kwaya tulifanikiwa kushiriki na wanakwaya
wenzetu wa Jimbo kuu la Dar Es Salaam siku ya jumatatu ya Pasaka Tarehe
06.04.2015. Ambapo maadhimisho hayo yaliongozwa na Mhadhama Kardinali Polycarp
Pengo na yalifanyika katika Parokia ya
Kipawa. Hivyo tunapenda kutumia fursa kutoa shukrani zetu za dhati kwa Baba
Paroko kwa kutuwezesha kushiriki katika adhimisho hilo.
D.
SALA
MAALUMU YA KIKUNDI
Jukumu hilo la kuandaa sala
maalumu, Kwaya imeandaa mapendekezo ya sala na inatakiwa ifanyiwe uhakiki na
maboresho kwa kuikabidhi katika kamati ya Liturujia na kamati kuipeleka kwa
Mapadre ili kuihakiki.
- UIMBAJI NA MUZIKI
Kwaya imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutekeleza mikakati yote iliyojiwekea kuhusu Uimbaji na Muziki kwa
kufanya yafuatayo:-
- Kundaa nyimbo za Vipindi mbalimbali Vya Liturujia ya Kanisa
- Kufanya Ziara za Uinjilishaji ndani ya Jimbo letu.
- Kuanzisha Darasa la kufundisha wankwaya Upimishaji.
- Kuendelea Kuhamasisha Watu mbalimbali kujiunga katika Utume huu wa Uimbaji ambapo kwa sasa tupo wanakwaya 55. Hivyo Bado tunahitajika kuhakikisha kuwa wanakwaya tulionao wanakuwa hai siku zote na Kuongeza wapya ili kufikia malengo yetu ya wanakwaya 70 kwa mwaka huu.
- KUJIUNGA KATIKA VIKOBA.
Kwaya tumefanikiwa kujiunga
katika mojawapo ya VIKOBA vinavyoendeshwa na WAWATA hapa Parokiani kwetu.
- KUTENGENEZA/KUNUNUA VITU NA KIVIUZA
Kwaya
imefanikiwa Kubuni Vazi la Familia ya Kwaya ambalo litavaliwa kwenye matukio
makubwa ya kwaya yetu Mf. Sherehe ya Maadhimisho ya Somo wa Kwaya n.k. Na
litavaliwa na Wanakwaya Wote, Walezi wa Kwaya, Marafiki wa Kwaya na Ndugu mmoja
wa karibu wa Mwanakwaya yaani Mke/Mme/Mtoto/Mlezi…. Ambapo vazi hilo tunapenda kulizindua rasmi siku ya
leo. Thamani vya Vazi itajumuisha gharama halisi ya Vazi na gharama nyingine
kuchangia utekelezaji na Maendeleo ya Kwaya hasa Mkakati wa Kurekodi Audio na
Video ambapo gharama zake ni Tshs.16,400,000/=
- MAHUSIANO
Katika kudumisha na kuboresha
Mahusiano kati ya Makundi yanayounda Familia ya Kwaya, Tumefanikiwa kuandaa
E-mail na Blog ya Kwaya ambayo
itatoa nafasi ya kushirikishana mambo mbalimbali kwa wakati, na pia kupokea
mapendekezo/maoni kutoka kwa watu mbalimbali.
- CHANGAMOTO ZA KWAYA.
- HALI NGUMU YA KIUCHUMI KWA WANAKWAYA
Hali ya kiuchumi kwa wanakwaya bado imekuwa tatizo kiasi
kwamba inapelekea hata uhudhuriaji wa mazoezi kuwa sio mzuri kutokana na pilika
za utafutaji riziki na hasa usio katika mfumo rasmi, kwani mara nyingi idadi
yetu huwa kubwa sana lakini wanakwaya hai ni wachache ambapo kwa sasa ni
wanakwaya 40.
- KUTOKUWA NA KINANDA CHA KUJIFUNZIA
Vyombo vya Muziki hasa kinanda cha kujifunzia pia ni tatizo
katika Kwaya yetu, hivyo kunyima fursa kwa wanakwaya hasa walio katika Darasa
la Muziki kujifunza.
- IDADI NDOGO YA WANAKWAYA WATU WAZIMA
Kuwa na Idadi ndogo ya wanakwaya Watu Wazima bado Kwaya
inaona kama ni tatizo kwani tunaamini kuwa iwepo wao utaweza kuimarisha na
kuboresha Kwaya yetu, kwani asilimia kubwa yao watakuwa na Makazi ya kudumu
katika Parokia yetu.
- MAPENDEKEZO
- FURSA YA KUWA NA MARAFIKI WA KWAYA
Kutokana na hii fursa ya uwepo wa Marafiki wa Kwaya tunaomba
mtusaidie katika kuhamasisha waamini mbalimbali ili waweze kujiunga na kwaya
yetu na pia kutusaidia mawazo mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi.
- MWISHO
Tunatoa shukrani zetu nyingi za
dhati Kwako Mgeni Rasmi, Baba Paroko, Mapadre, Walezi na Marafiki wote kwa moyo
wenu wa kujitoa na kushiriki nasi katika Tafrija hii fupi. Tunasema Asante na
tunawatakia Matashi Mema na Mungu awabariki Sana.
WENU KATIKA UTUME WA KRISTO.
Imeandaliwa na
Imeidhinishwa na
…………………………..
……………………………
SIBILINA KIMARO
LUAMBANO PATRICK
Katibu wa kwaya
Mwenyekiti wa Kwaya
No comments:
Post a Comment