KATIBA

PAROKIA YA BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMEL - BUNJU
KWAYA YA BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMEL
JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM
P. O. Box 167, Dar es Salaam
MOBILE: +255784 799 455

KATIBA YA KWAYA YA BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMELI.
UTANGULIZI:

IMANI

Kwaya inaamini kwamba kwa kuimba vizuri wanakwaya husali na kutangaza neno la Mungu. Pamoja na kumtukuza Mungu. Pia Mwanakwaya anayeimba vizuri, anasali mara mbili zaidi ya kawaida.
Katiba hii imueundwa mwaka 2006. Katiba hii imerekebishwa mwaka 2009 na 2010 kwa mara ya pili.
SEHEMU YA KWANZA:

1.1  JINA LA KWAYA
    (a)    Kwaya hii itaitwa Bikira Maria wa Mlima Karmeli
    (b)   Somo kwa Kwaya Bikira Maria wa Mlima Karmeli
    (c)    Makao makuu ya Kwaya ni kanisa Katoliki Kigango cha Mt. Joseph Bunju.

1.2  MADHUMUNI YA KWAYA
   (a)    Kuwaongoza na kuwashirikisha wakristo katika ibada ya Misa Takatifu kulingana na taratibu za kiluturujia. 
   (b)   Kumtukuza na kumsifu Mungu kwa nyimbo
   (c)    Kulinda na kudumisha Imani ya Kanisa Katoliki na moyo wa upendo moyoni mwetu.
   (d)   Kueneza na kuhubiri neno la Mungu kwa nyia ya nyimbo.
   (e)    Kujenga na kuimarisha moyo wa upendo miongozi mwa wanakwaya wakristo wa Parokia yetu na Parokia nyingine.
   (f)    Kujenga na kuimarisha uhusiano mwema na Kwaya nyingine Jimboni, Tnzania nzima na Duniani kote.

1.3  SIFA ZA MWANAKWAYA.
    
    (a)    Mtu yeyote ambaye ni Mkatoliki mwenye umri usiopungua miaka kumi na tano (15) na kuendelea na mwenye akili timamu anaweza kujiunga na Kwaya.  
   (b)   Awe na uwezo wa kuimba na kupenda kuimba.
   (c)    Awe mwenye kujiheshimu, asiyefanya matendo kinyume na maadili ya kikatoliki.
   (d)   Awaheshimu viongozi wa kanisa, Viongozi wa Kwaya na wanakwaya wenzake  
   (e)    Awe asiyetengwa na kanisa Katoliki au kuwa na kizuizi chochote cha Sakramenti au iwapo anacho basi awe katika jitihada za kuondokana nacho.

1.4  MASHARTI YA KWAYA

    (a)    Usajili – Muda wa usajili ni miezi mitatu(3) baada ya hapo atasajiliwa au kutosajiliwa kutokana na mwenendo wake, anaweza kuongezewa muda wa usajili kwa maandishi.
   (b)   Siku za mazoezi zifuatwe ipasavyo yaani Jumanne, Ijumaa na Jumamosi kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 12:30 jioni, pamoja na misa za jumapili na siku nyingine za dharula.
   (c)    Asiyehudhuria mazoezi kwa wiki nzima akae nyuma ya benchi la Kwaya.
  (d)   Hapatakuwa na mchango binafsi-mchango unaotolewa na mwanakwaya asuichukulie kwamba anajiwekea akiba
   (e)    Mwanakwaya akishindwa kuhudhuria kwenye Kwaya atapewa onyo la mdomo wiki mbili, zaidi ya wiki mbili atapewa barua, ikiwa unashindwa kwa zaidi ya mwezi andika barua.

1.5  MASHARTI YA MWANAKWAYA

   (a)    Mwanakwaya atakaye shindwa kuhudhuria au kuwa karibu na kikundi bila taarifa maalumu ndani ya mwezi mmoja(1) ataandikiwa barua ya kumtaka ajieleze au ya kumpa onyo au atasimsmishwa.
   (b)   Mwanakwaya akiwa na nidhamu mbaya ndani na nje ya kikundi(atasimamishwa au kufukuzwa)
  (c)    Mwankwaya akiwa ni chanzo cha vikwazo vingi ndani ya kikundi mf. Lugha chafu zinazoleta mvurugano katika kikundi, ataadhibiwa kikatiba.
  (d)   Mwanakwaya atasimamishwa kujihusisha na uimbaji anapopatikana na tuhuma ndani na nje ya Kwaya, uchunguzi ukikamilika ataarifiwa kuendelea au kutoendelea na Kwaya.
   (e)    Mwanakwaya analazimika kutoa michango yote husika katika Kwaya.

1.6  WAJIBU WA MWANAKWAYA
  (a)    Mwanakwaya anawajibika kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za Kwaya kufuatana na utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa katiba hii.
   (b)   Kuhudhuria ibada na hafla zote zitakazoihusisha Kwaya hii.
   (c)    Kuwa tayari kujikosoa, kukosoa na kukosolewa.
   (d)   Kuwa  mfano wa tabia njema na upendo kwa wote.
   (e)    Kuhudhuria mazoezi bila kukosa. 
   (f)    Kila mwanakwaya anawajibika kwa kutunza mali za Kwaya mf. Sare
   (g)   Kurudisha mali za Kwaya pale anapoacha au kuhama.
  (h)   Kuwa na sare(kujinunulia sare) zilizonunuliwa kwa ubinafsi, sare zilizonunuliwa na Kwaya atagawiwa.
    (i)     Kuheshimu sare za Kwaya na siyo kuvaa hovyo hovyo.
    (j)     Kulipa ada na michango husika.

1.7  HAKI ZA MWANAKWAYA
Mwanakwaya ana haki ya:- 
    (a)    Kuwa huru kutoa malalamiko, shida au kujitetea iwapo ametuhumiwa, atafanya hivyo katika  kikao kinachohusika pindi atakaporuhusiwa kufanya hivyo.
    (b)   Kuongea na Kiongozi yeyote juu ya malalamiko kwa kufuata taratibu zilizopangwa.
    (c)    Kufahamu mapato na matumizi ya Kwaya
    (d)   Kuchagua au Kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Kwaya.
    (e)    Kutoa maoni yake pale anapohusika.

1.8  KUSIMAMISHWA KWAYA
Mwanakwaya atasimamishwa kuendelea na Kwaya:- 
   (a)    Endapo ameonekana kuwa na kizuizi cha muda mrefu ambacho hayuko katika hatua za kuondokana nacho.
   (b)   Endapo kiongozi au mwanakwaya yeyote atatumia vibaya fedha za Kwaya bila idhini ya Kwaya, pia atatakiwa kulipa fidia ya fedha atakazokuwa anadaiwa kulingana na maamuzi ya kikao cha Kwaya.
NB
·         Kabla ya kusimamishwa apewe onyo mara tatu, onyo la kwanza kwa mdomo la pili kwa barua na baadaye atasimamishwa rasmi kwa barua.
·         Kmati tendaji iwashauri wale wenye vizuzi kisakramenti ili waondokane navyo.

1.9  KUACHA KWAYA
Mwanakwaya anaweza kuacha Kwaya iwapo:-
    (a)    Atatoa taarifa ya kimaandishi kwenye Kwaya kwa sababu zake zilizo na msingi, taarifa atoe mwezi mmoja kabla.
    (b)   Mwanakwaya anaumwa au kufariki

2.0 KUACHISHWA KWAYA

Mwanakwaya ataachishwa Kwaya :-
    (a)    Ikiwa hatatimiza wajibu wake kama mwanakwaya na masharti ya Kwaya ipasavyo
    (b)   Ikiwa atapatikana na makosa makubwa ya kinidhamu ndani na nje ya Kwaya
  (c)    Kwa makosa yenye uzito wa kawaida, mwanakwaya aliyefanya kosa mara tatu(3) kabla ya kuachishwa , makosa na maonyo yatatumwa katika kipindi cha miezi sita(6)
  (d)   Mwanakwaya atakayepatikana na makosa madogomadogo atachukuliwa hatua na kamati ya nidhamu kwa kuonywa kwa mdodmo, na mara ya pili ataandikiwa barua na nafasi ya kujieleza na ya tatu kamati tendaji itatoa maamuzi ya mwisho.
  (e)    Kwa makosa ya hali ya juu yenye kuleta fedheha kwa Kwaya, mwanakwaya aliyefanya kosa atafukuzwa mara moja.

2.1 SEHEMU YA PILI: MUUNDO WA UONGOZI

2.1. KIONGOZI

Kiongozi wa Kwaya ni mwanakwaya yeyote mwenye dhamana yoyote aliyechaguliwa au kuteuliwa kikatiba.

2 comments:

Aleluya Kuu

Jesus Christ Your My Life